KUBALI KUWAPOTEZA USONGE MBELE


Katika maisha tunayo ishi ukijua Kuna watu lazima tukubali kuwapoteza ili mambo mengine yaendelee pia wapo ambao lazima tuwakaribishe ktk maisha yetu ili wawe daraja kufikia ndoto zetu.

Kuna watu unao kutana nao kupitia matendo na tabia zao umepata funzo kubwa katika maisha... Haijalishi wamekuumiza au kukufurahisha

Wapo watu ambao siku zote watakuumiza lakin utajifunza kitu kupitia maumivu waliyo kuachia

Wapo watu ambao watakujenga kiakili na kukufanya ujitambue na uwe mtu jasiri.... Kupitia wao utajifunza kujitegemea ktk maamuzi na maisha...

Siku zote amini kuwa kila mtu unae fahamiana nae katika maisha yako awe mbali au karibu,huyo ni sehemu ya watu muhimu katika maisha yako. Mthamini kila mmoja na kumuona anafaa kwa nafasi yake.

Usilazimishe mtu aendelee kuwepo katika maisha yake kama mda wake kutoka umefika.. Usiumizwe na HISTORIA yenu kuwa urafiki wenu umetoka mbali sana.... Usifikirie watu wangapi walifahamu mahusiano yenu... Jali furaha na Amani ya moyo wako tu...

Ukiona kamba uliyoishikilia inakuuchubua mikono vyema uiachie ili uwe salama zaidi

Post a Comment

0 Comments