Na. .Amon Mtega,Namtumbo.
MBUNGE wa Viti maalum Mkoani Ruvuma Jacqueline Ngonyani (Msongozi) amewaahidi wanawake wa Mkoa huo kuendelea kuungana kutafuta fursa mbalimbali za kimaendeleo ili kuimarisha uchumi kwenye jamii.
Akipokelewa na wanawake wa Wilaya hiyo ambao ni wajumbe wa baraza la UWT na kumpeleka eneo la ujenzi wa nyumba ya katibu wa Jumuiya hiyo Mbunge huyo ameahidi kutoa sh.Milioni mbili (SH.2,000,000.)kwaajili ya kuendeleza ujenzi huo ambapo kwenye Jumuiya ya Wazazi ameahidi Sh. Laki tano(sh.500,000.)pamoja na Jumuiya ya Vijana UVCCM nayo ni Sh.Laki tano(sh.500,000.)ambazo Jumuiya hizo nazo zina ujenzi wa nyumba za makatibu wao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Namtumbo Agrey Mwansasu amempongeza mbunge huyo kwa kazi anazozifanya kwenye jamii nzima huku akisema chama Wilayani humo kinatambua mchango wake kwenye jamii.
0 Comments