HIZI HAPA SABABU ZA KUVUNJIKA MAHUSIANO AU NDOA


Kuna muda kila mmoja anajitunza na kujiheshimu pasipo kuwa na wazo la kumsaliti mwenzake.. Lakini Mawasiliano yakiwa finyu yaani mmoja yeye ndo wa kupiga na kutuma sms huku mwingine KAZI yake kujibu napo mpaka ajisikie asipo tafutwa nae anakaa kimya

Heshima ikikosekana.

Sawa unampenda sana na hutako kumuacha lakini inapofika hatua husikilizi mawazo yake,Una mchukulia kama mtoto, Huoni shida kumtolea lugha chafu hata kumpiga.

Pesa ikikosekana.

Pesa ina nafasi yake katika mahusiano japo ili iweze kutatua shida ndogo ndogo na kusaidiana.. Inapokosekana ni tatizo.

Uongo na kukosa uvumilivu.

Unaweza achwa au kumuacha mtu sababu ya kukosa uaminifu na uwazi katika mambo yenu.. Anaweza asiwe msaliti lakini akawa muongo kupindukia... Uwongo unapogundulika huwa maumivu kwa aliyedanganywa... Umesema una gari ila huna
Umesema utaishi nae kwa hali yoyote anakuletea mimba unakataa.

Hivyo tukae tukijua kuwa

KISICHO RIDHIKI HAKILIKI

Kama unaona kuna kinacho zuia furaha yako kwa mtu uliye nae fanya uamuzi wa busara kujiweka pembeni kabla hujaumia au kumuumiza zaidi mbeleni.

Mawasiliano mara kwa mara pande zote
Uvumilivu
Uaminifu
Kusaidiana
Maelewano
Upendo

Ndiyo nguzo katika mahusiano
Kimoja kikikosekana basi mda wowote mtasumbuana

Hakuna anayependa kuumizwa na mapenzi japo wapo wanaofurahia kuwaumiza wengine

Post a Comment

0 Comments