![]() |
Mkurugenzi msaidizi wa kituo cha Swacco ,Anna Mugenya akielezea changamoto ya vifaa vya michezo kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho. |
WADAU mbalimbali wametakiwa kujitokeza kusaidia vifaa mbalimbali vikiwemo vya michezo kwa Watoto wanaolelewa (Yatima) katika kituo cha Songea Women and Children Care Organisation (SWACCO) kilichopo kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ili kuibua vipaji kwa watoto hao.
Akizungumza mkurugenzi msadizi wa kituo hicho Anna Mugenya amesema kuwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho wengi wao wamekuwa na vipaji mbalimbali vikiwemo vya michezo huku shida kubwa ya kuvivumbua vipaji hivyo ni ukosefu wa vifaa hasa vya michezo.
Kufuatia hali hiyo mkurugenzi msaidizi huyo anawaomba wadau kujitokeza katika kufanikisha kuvipata vifaa hivyo ambavyo vitakavyowafanya watoto hao kuvitambua vipaji vyao tofauti na sasa wamekuwa wakitumia vifaa visivyo rasmi jambo ambalo wamekuwa wakihisi kama wanabaguliwa .
Anna amevitaja vipaji vilivyopo kwa watoto hao kuwa ni Uimbaji,uchezaji wa mpira wa aina zote,pamoja na michezo mingine mbalimbali ambayo inafanya watoto wajengeke kuwa na Afya njema licha ya kuwa na vipaji .
Naye mmoja wa watoto hao Alukwini Ndauka amesema kuwa wamelelewa toka watoto wadogo katika kituo hicho hivyo wanawaomba wadau wawasaidie vifaa vya michezo ili nao waweze kucheza michezo kama watoto wengine.
![]() |
Watoto wa Swacco wakitumia vifaa vya miziki walivyojitengenezea wenyewe kwa lengo kuimba na kusaka vipaji vyao. |
Mtoto Alukwini Ndauka amesema kuwa licha ya msaada wa vifaa vya michezo lakini bado wanauhitaji wa vitu mbalimbali ikiwemo ndala za kuogea .
0 Comments