MZOZO WA UKRAINE NCHI ZA MAGHARIBI ZINAWEZA KUFANYA NINI



Nato imeweka ndege za kivita katika hali ya tahadhari lakini muungano wa Magharibi umeweka wazi hakuna mipango ya kutuma wanajeshi wa kivita nchini Ukraine yenyewe. Badala yake wametoa washauri, silaha na hospitali za kutumiwa vitani . Wakati huo huo, wanajeshi 5,000 wa Nato wametumwa katika mataifa ya Baltic na Poland. Wengine 4,000 wangeweza kutumwa Romania, Bulgaria, Hungaria na Slovakia.

Badala yake, nchi za Magharibi zinalenga uchumi wa Russia, viwanda na watu binafsi.

• Umoja wa Ulaya umeahidi kuwekea vikwazo Urusi katika masoko ya mitaji na kukata tasnia yake kutokana na teknolojia ya kisasa zaidi. Tayari imewawekea vikwazo wabunge 351 waliounga mkono Urusi kutambua maeneo yanayodhibitiwa na waasi.

• Ujerumani imesitisha uidhinishaji wa bomba la gesi la Nord Stream 2 la Russia, uwekezaji mkubwa wa Urusi na makampuni ya Ulaya.

•Marekani imesema itaitenga serikali ya Urusi kutoka kwa mashirika ya fedha ya nchi za Magharibi na kuwalenga "watu" wa ngazi za juu.

• Uingereza inasema benki zote kuu za Urusi zitafungiwa mali zao, huku watu binafsi na mashirika 100 yakilengwa; na shirika la ndege la taifa la Urusi Aeroflot pia litapigwa marufuku kutua nchini Uingereza

Ukraine imewataka washirika wake kuacha kununua mafuta na gesi ya Urusi. Mataifa hayo matatu ya Baltic yametoa wito kwa jumuiya nzima ya kimataifa kutenganisha mfumo wa benki wa Russia na mfumo wa malipo wa kimataifa wa Swift. Hilo linaweza kuathiri vibaya uchumi wa Marekani na Ulaya.

Jiji la Urusi la St Petersburg halitaweza tena kuandaa fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka huu kwa sababu za kiusalama. Shirikisho la soka barani Ulaya Uefa pia linapanga hatua zaidi.

source :BBC

Post a Comment

0 Comments