Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ametangaza kuwa kuanzia machi mwaka huu 2022 serikali yake itaanzisha mafao ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa lengo la kulinda utu wa vijana ambapo kila kijana katika taifa hilo linalokadiriwa kuwa na watu milioni 45 atapata dinari 13000 ambazo ni sawa na Dola 92 na sawa na shilingi laki 213,000 ambapo malipo yataendelea mpaka muhusika atakapopata ajira.
Malipo haya ya kila mwezi yataambatana na huduma nyingine kama vile matibabu bure huku kodi kadhaa katika baadhi ya bidhaa za walaji zikiondolewa kutoka kwenye malipo hayo ambayo ni sehemu ya bajeti ya mwaka 2022.
Taifa hilo la Afrika Kaskazini linapambana na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa karibu asilimia 15 pamoja na kwamba nchi hiyo ni wauzaji wakubwa wa gesi barani Afrika ambapo asilimia 90 ya mapato yake yanatokana na mafuta na gesi
0 Comments