Mfano wa mkono wa mamba na mjusi
Mkazi mmoja wa Kitongoji cha Mbyaso, Kijiji cha Mpunguti, Kata ya Ikama wilayani Kyela mkoani Mbeya, aliyefahamika kwa jina la Maria Mwakila (26), amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutokwa na mjusi sehemu za siri alipokwenda kujisadia haja ndogo.Wiki tatu zilizopita, binti huyo aliripotiwa kujifungua mkono wa mamba na kuzua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo ambapo Ilidaiwa kuwa alikuwa na ujauzito wa miezi mitatu na alitibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela baada ya kukumbana na mkasa huo.
Siku 18 baada ya kupata matibabu hayo, jana majira ya saa mbili asubuhi, alipokwenda kujisaidia haja ndogo, alidai ulitoka mjusi ukiwa na kucha mkiani.
Akizungumzia tukio hilo Mume wa binti huyo ` amedai kuwa baada ya kupata ujauzito, mke wake alikumbana na matatizo mengi ikiwamo kuugua mara kwa mara na ilipotimu miezi mitatu ya ujauzito huo, alianza kujisikia dalili za uchungu na walipomuwahisha hospitalini alipona na kurejea nyumbani lakini siku hiyo hiyo aliyotoka hospitalini, akiwa sebuleni, alijisikia kama ameshikwa na haja ndogo, alipofika eneo la kujisitiri, alijikuta akitokwa na mkono wa mamba huku damu nyingi ikimtoka.
Ameongeza kuwa baada ya tukio hilo ilibidi akimbizwe hospitalini na kupatiwa matibabu ikiwa ni pamoja na kusafishwa tumbo ambapo waliondoa uchafu uliokuwamo na baada ya wiki tatu akiwa katika hali safi na salama akajikuta anajisaidia mjusi ulio na mkia wenye kucha.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, amesema ni tukio la kwanza kutokea katika eneo lao na pia waliposikia mwanamke amejifungua mkono wa mamba waliona ni jambo la kawaida kwa kuwa maeneo mengi huwa yanatokea lakini tukio la pili walipolisikia walishikwa na butwaa ndipo walipoitisha kikao ili wajue tatizo na kulitafutia ufumbuzi.
Akizungumzia hali hiyo, Maria amesema anamwachia Mungu, akiamini ipo siku atajifungua mtoto wa kawaida asiyekuwa na dosari.
Chifu Mkuu wa Kijiji hicho, Magojanya Mwaluswa, amesema wamekemea kitendo hicho na kushauri familia zinazovutana na kuwa kile wanachoamini ni kiini cha tatizo, zimalizane kwa kuwa kijiji hicho na vitongoji vyake havina historia ya matukio hayo.
0 Comments