WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO


Ruvuma,

TEMBO saba (7) wameuawa katika matukio mawili tofauti Mkoani Ruvuma huku kila Tembo akiwa na Thamani ya USD 15,000 sawa na pesa za kitanzania Tsh 242,550,000.
Akizungumuzia tukio la kuuawa kwa Tembo hao kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo amelitaja tukio la kwanza kuwa lilitokea Mei mosi mwaka huu majira ya saa tano usiku katika maeneo ya Hanga Monastery Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma ambapo walikamata meno ya Tembo matano (5)yenye uzito wa Kilogramu 44 yenye thamani ya Tsh,103,950,000,ambapo katika tukio hilo watuhumiwa walifanikiwa kutoroka.


Kamanda Konyo amelitaja tukio la pili kuwa lilitokea Mei kumi mwaka huu majira ya saa mbili usiku katika Kijiji cha Milonde -Kiuma Wilaya ya Tunduru ambapo walikamata meno ya Tembo mazima manne na vipande vinane vyenye uzito wa 20.4 Kilogramu vyenye thamani ya Tsh.138,600,000 huku watuhumiwa watatu wa tukio hilo wakikamatwa ambao ni Said Awadi (25) Hassan Hakimu (36)Zachalia Gafi (22) ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani.


Konyo amesema kuwa kufuatia matukio ya kukamatwa kwa meno ya Tembo kumesababisha kuuawa kwa Tembo saba Jambo ambalo limesababisha hasara kwa Taifa na kuharibu urithi wa vizazi vijavyo.


Kwa upande wake kamishna mwandamizi wa Mamlaka ya wasimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) kamanda wa uhifadhi kanda ya kusini Mashariki Abraham Jullu amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wataendelea kuwasaka watu ambao wamekuwa wakiharibu rasilimali za Taifa.


Post a Comment

0 Comments