KWANINI ALIE KISA WEWE??
KWA NINI ULIE KISA YEYE ??
KAKA na DADA katika mahusiano ni kama tupo safarini kwa maana ajali inapotokea hujui ni wapi na sababu ni ipi na madhara yake yatakuwaje.
MAPENZI yamekuwa kama mchezo wa kubahatisha hujui mkweli na muongo nani
Usiumize wengine kisa huko nyuma nawe kuna mtu ulimpenda ila aka kuumiza sana na mpaka leo kakufanya uyachukie mapenzi.
Kumbuka usihukumu wengine kwa sababu zako binafsi za chuki na hasira
Ni kweli waweza kuwa unauguza maumivu na majeraha ya nyuma lakini isiwe sababu ya wewe kuwafanya wengine walie kwa ajili yako.. Aliye kuumiza ni mmoja usihukumu wengine wasiohusika.
Kuna walioumizwa zaidi yako lakini waliomba Mungu mpaka sasa wanaishi na familia zao. Kila mmoja ana historia ya maumivu katika mahusiano. Tunatofautiana katika kuzionesha na kuficha
"Wanawake wote malaya tu hawana mapenzi ya dhati ..dawa yao ni kupiga na kuacha na mimba"
"Wanaume wote ni mbwa tu hawaridhiki ..dawa yao ni kuwachuna tu"
Hayo ni maneno tunayotoa pale Mioyo yetu inapojaa chuki na ghadhabu.. Lakini ukifuatilia sio kweli. Binadamu hatuwezi kufanana kila Mtu na imani na tabia yake..
Unapo sema WANAWAKE wote wanapenda tu pesa kuna wenzako wanaendelea kuchumbia na kuoa .. Unapo sema WANAUME wote wanatamaa mda huo huo wengine wanazidi kuoa ....
Ifike wakati tusiendeshwe na roho za chuki na kisasi sababu ya mambo tuliyofanyiwa nyuma. Siku zote ishi katika malengo yako kwa mara ya kwanza ulipojiingiza katika uhusiano kabla ya kuvunjika.. Ulitarajia Uwe BABA au MAMA bora,ulitaka uwe na familia yenye furaha ,Bado hujachelewa usikiri kushindwa kabla hujajaribu tena.
Ndoto zako zilifeli kwake ila ukiwa na mwingine zinaweza kufanikiwa. Hata tunao washuhudia makanisani wakifunga ndoa utakuta alishawahi kuumizwa hata mara 5., Tusikate tamaa sababu ya maumivu na visasi.
Ndoto yako haikuwa uishi na mtoto bila MAMA au BABA bali muwe wote. Hata kama leo una mtoto bado unayo nafasi kupata mke au mume. Kulingana na unavyo jitunza
Ukitaka kuishi kwa furaha usimfikirie aliye kuumiza bali waza yaliyo mbele yako.. Huwezi kutatua tatizo kwa kulikimbia lazima upambane nalo. Maumivu yako yatapungua endapo utapata wa kukusahaulisha.
Siku zote anaeumia ni yule mwenye upendo wa dhati na kujali.. ..Tuishi kwa kujali yetu na sio ya wengine. Aliye kutenda saizi yupo na familia yake hana mda nawe nawe tafuta yako. Anapo kuona bado SINGLE GIRL au BOY kwake ni ushindi anajiona huwezi mpata zaidi yake na anaamini bado unampango kurudiana nae. Siku ukipata atakayekuheshimu na kukupenda halafu ukanawili basi ataumia na kuanza kuja kuomba msamaha.
Bado we mrembo..bado we kijana bora usikate tamaa bado wapo wengi wanaofikiria kuoa na kuolewa.
Mshirikishe Mungu akupe ujasiri wa kuanza upya safari ya mahusiano ,akupe kibali kuacha machafu na kuanza upya..
Miongoni mwa wanaokuzunguka yupo anae tamani siku moja aishi nawe
0 Comments