Kafara yatajwa chanzo ukatili Geita


Imeelezwa kuwa tathmini inaonyesha dhana potofu ya mauaji ya ndugu ili kupata mali ni miongoni mwa vichocheo vya matukio ya  kikatili katika mkoa wa Geita 

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Safia Jongo amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Lwamugasa,kata ya Lwamugasa wilayani Geita ambapo amesema jeshi la polisi mkoani humo limejipanga kukomesha vitendo hivyo

Amesema vitendo hivyo hutokea kutokana na watu kuaminishwa kwamba wakifanya mauaji ya ndugu watapata utajiri jambo ambalo limeendelea kuchafua taswira ya mkoa huo 

Post a Comment

0 Comments