Februari 17, viongozi wa Afrika Mashariki waliwataka makundi yote yenye silaha yasiyo ya serikali kuondoka katika eneo wanalokalia mashariki mwa Congo ifikapo Machi 30.
Kuondoka huko kulikusudiwa kufanyika katika awamu tatu, na awamu ya kwanza kuanza Februari 28.
Lakini waasi wa M23 waliendelea kusonga mbele katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC siku ya Jumanne.
Siku ya Jumatatu, kundi hilo linaloongozwa na Watutsi liliteka mji wa Mweso, takriban kilomita 100 magharibi mwa mji mkuu wa jimbo la Goma.
Kiongozi wa jumuiya ya kiraia katika eneo hilo Alphonse Habimana aliiambia AFP siku ya Jumanne kwamba M23 inadhibiti mji huo wenye watu wapatao 30,000.
SOURCE: VOA
0 Comments