USIPOTEZE MUDA KUPIGANA VITA VISIVYOKUINUA



Usipoteze muda kushindana wala kujibizana na watu wasiokuwa na mchango chanya juu ya maisha yako..

Usiruhusu mambo yaliyoshinda nguvu na akili zako yakufanye uwe na uchungu na huzuni nayo.

Kumbuka hata kama wewe ni mwema kiasi gani, sio kila mtu atakukubali,Kuna wakati hata marafiki zako wanaweza wakakuchukia bila sababu lakini hilo lisikufanye uwe na uchungu hata mpenzi uliyemuamini na kumsubiri kwa muda mrefu kesho unasikia anaoa au kuolewa wala usi simame kumlilia haitakusaidia

Kuna wakati hata ndugu zako mliozaliwa nao wanaweza kukuchukia kwa sababu mafanikio yako yanakuwa tishio kwao kama Yusufu na kaka zake.

Kuna wakati wafanyakazi wenzako wanaweza kukuchukia kwa sababu unafanya zaidi yao.

Kuna wakati watumishi wenzako wanaweza wakakuchukia tu kwa sababu huduma yako inazidi kuongezeka kuliko zao.

Lakini katika yote, usikubali chuki zao zipenye ndani ya moyo wako,Usikubali uchungu wao uingie ndani yako na kukuzuia kutimiza ndoto zako

Kumbuka kuwa kuna watu hata kama ufanye mema gani kwao hawatakaa waone hayo mema,ndivyo walivyo! Kuwa na amani na hilo wala lisisumbue akili zako.

Hata kama hawakupendi, hiyo haikuhusu na sio sababu ya kukufanya usitimize ndoto zako .

Simama kwenye nafasi yako bila kutetereka na bila kutishika na maneno yao, Simama kwenye nafasi yako kama Nehemia na endelea kutimiza kusudi la Mungu juu yako bila kujali mashambulizi ya maneno yao.

Furahi wakati wote katika mazingira yote na utaona vile Mungu atakavyokuinua na kukufanikisha mbele ya macho yao.

Fanya mashambulizi yao yawe chachu ya kukusukuma kufanya zaidi na sio kukudhoofisha hakika UTASHINDA.

Post a Comment

0 Comments