KATIKA kuupokea mwaka 2022 na kuuaga mwaka 2021 Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Ruvuma kimetumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Akitoa pongezi hizo mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amesema kuwa mkoa wa Ruvuma unatambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuwaletea maendeleo Wananchi wake hivyo anatakiwa kuungwa mkono.
![]() |
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Ruvuma Oddo Mwisho akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa alinayoifanya ya kuwaletea maendeleo Wananchi wake. |
Mwisho akizungumza na vyombo vya habari mkoani humo amefafanua kuwa hivi sasa miradi mikubwa ikiwemo ya ujenzi wa madarasa yamejengwa Nchi nzima ni kwa sababu ya ubunifu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Katika hatua nyingine mwenyekiti Mwisho amewataka wakazi wa mkoa wa Ruvuma kuwapuuza watu wanaozusha mambo mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii wanaoikashifu Serikali bila sababu za msingi.
Amesema kuwa watu hao wamekuwa wakitengeneza vitu vya kutugawa watanzania kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo amedai kuwa halikubaliki .
Hata hivyo Mwisho amewaomba wakazi wa mkoa huo kuzitumia vema mvua za msimu huu kwa kuzalisha mazao kwa kuwa mvua inaonyesha dalili kwa mwaka huu zitakuwa chache tofauti na miaka mingine.
Licha ya mwenyekiti huyo kuwataka Wananchi wa Ruvuma kutumia vema mvua za msimu huu lakini pia amewataka kutunza vyakula (Mahindi) kwa kuhifadhi vizuri na kuacha tabia ya kuuza yote,huku akiiomba Serikali kuona namna ya kuweka ruzuku kwenye pembejeo (Mbolea) ili mkulima aweze kununua kwa bei ya chini .
0 Comments