Vifo,majeruhi waongezeka mafuriko Manyara


Idadi ya vifo vya watu kutokana na mafuriko yaliyotokea katika mji wa Katesh, wilaya ya Hanang mkoani Manyara imeongezeka na kufikia watu 49 baada ya kupatikana miili huku zoezi la uokoaji likiwa linaendelea.

Naibu waziri wa Afya Mhe. Godwin Mollel ametoa taarifa hiyo leo  akisema idadi ya majeruhi walioko katika hospitali zote mkoani Manyara imefikia 93 na kwa sasa shule za msingi Hanang, Katesh na Dumanang zitatumika katika kuhifadhi waathirika wa mafuriko hayo.

Mhe. Mollel amesema kuwa wizara hiyo imeratibu upatikanaji wa timu za madaktari kwa ajili ya kuongezea nguvu katika hospitali za mkoa wa Manyara

Post a Comment

0 Comments