13 wafariki ajalini Singida

 

Watu 13 wamefariki dunia na wengine 25 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Mwanza kugonga kichwa cha treni katika makutano ya barabara na reli eneo la Manyoni mkoani Singida.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 10 Alfajiri.

Ajali hiyo imehusisha basi la abiria ambalo ni mali ya kampuni ya Ally's lenye namba za usajili T178 DVB ambalo limegonga kichwa cha treni kilichokuwa kikisafiri kutoka Itigi kuelekea Manyoni mkoani Singida na tayari Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekekwa katika hospitali za Itigi na Manyoni kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments