Watahiniwa 31 Darasa La saba wafutiwa Matokeo


Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limefuta Matokeo ya watahiniwa 31 ambayo ni sawa na asilimia 0.002 ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi (PSLE) iliyofanyika septemba 13 na 14 mwaka huu 2023.

Katibu mtendaji wa NECTA Dr. Said Mohamed amesema Baraza limefungia vituo vya Mitihani viwili ambavyo ni Twibhoko na Graiyaki vyote vya halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara baada ya kuthibitika kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo.

Baraza Hilo pia limeziandikia barua za onyo vituo vinne vya Mitihani ambavyo ni Mother Of Mercy,St.Marys Mbezi Beach vilivyopo Halmashauri ya Kinondoni mkoani Dar es salaam,Charm Modern kilichopo Halmashauri ya Karatu mkoani Arusha na Morotonga cha Halmashauri ya Serengeti mkoani Mara baada ya kubainika vilijaribu kujihusisha na vitendo vya kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo.

Vituo hivyo vitakuwa chini ya uangalizi wa Baraza la Mitihani mpaka Baraza litakapojiridhisha kuwa vituo hivyo ni salama Kwa iendeshajo wa mitihani ya Taifa.

Matokeo ya Darasa La saba yametangazwa hii Leo Novemba 23,2023 Jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa NECTA Dr,Said Mohamed 




Post a Comment

0 Comments