Wawili wahofiwa kufariki ajali makutano Musoma, Tarime


Watu wawili wanahofiwa kufariki dunia baada ya roli walilokuwemo kupoteza mwelekeo na kuingia mtoni kisha kulipuka katika eneo la makutano ya barabara ya Mwanza- Tarime- Musoma.

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Disemba 4 saa 12 asubuhi katika eneo la makutano wilayani Butiama mkoani Mara 

Watu hao ni dereva na kondakta ambao bado hawajajulikana majina yao na sehemu waliyokuwa wameenda kutokana na kushindwa kutoka nje baada ya gari kutumbukia mtoni kulipuka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Salum Morcase amesema gari hilo lilikuwa linatoka Mwanza na uchunguzi wa awali wamebaini kuwepo kwa mapipa ambayo yanadhaniwa kuwa na kemikali ingawa haijajulikana kulikuwa na kemikali za aina gani.

Post a Comment

0 Comments