Idadi ya watu wa familia Moja ya Lazaro Sanabanka waliopoteza maisha Kwa kile kinachodaiwa kula chakula chenye sumu usiku wa Novemba 13,2023 katika Kijiji cha Nyakanazi kata ya Rusahunga Wilayani Biharamlo mkoani Kagera imeongezeka kutoka watu watano (5) Hadi sita (6) baada ya mtoto Josephina Juma (5) aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Biharamlo kufariki hii Leo.
Watoto wengine waliofariki Dunia ni Melisiana Razaro(11), Melina Razaro (9),Bryan Ezekiel (3),Kahindi Samson (9) na Happines Razaro (12) aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Muungano.
0 Comments