Mabaki ya mwili wa mwanamke yakutwa na mafundi,Mume atuhumiwa kuhusika


Tukio la kustaajabisha limetokea katika Mtaa wa Nyamihimbi Kata ya Somanda Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, baada ya mabaki ya mwili wa mwanamke kukutwa ukiwa umefukiwa kwenye shimo.

Mwili huo umegunduliwa na Mafundi ujenzi, ambao walikuwa wakichimba msingi wa Nyumba kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Kwa mujibu wa Maelezo ya Mwenyekiti wa Mtaa na Mtendaji wa Kata, eneo hilo lilikuwa mali ya Juma Piteer ambaye alikuwa amejenga nyumba tope na aliishi hapo na mke wake aliyeitwa Suzan.

Ilielezwa kuwa baadaye Juma aliuza eneo hilo hivi karibuni, alimuuzia mwananchi mmoja ambaye ndiye alikuwa anataka kuanza ujenzi, baada ya kuuza Juma alihamia eneo jingine.

Eneo ambalo mwili umekutwa, imeelezwa kuwa ndipo Kilipokuwa chumba cha Juma na Mke wake wakati wanaishi hapo.

Kwa mujibu wa wataalumu wa Afya waliofika eneo hilo, wakati mabaki yakifukuliwa wameeleza kuwa mwili huo ulikuwa na muda wa zaidi ya mwaka mmoja toka umezikwa.

CHANZO:GLOBAL TV

Post a Comment

0 Comments