Jeshi la polisi mkoa wa Tabora linamshikilia
Rayson Agnelusi Duwe muuguzi msaidizi daraja II (ANO) katika hospitali ya
Wilaya ya Sikonge, kwa kosa la kumbaka mama mgojwa mwenye ujauzito wa miezi
tisa baada ya kumchoma sindano yenye dawa ya usingizi.
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Tabora ACP.
Richard Abwao akitoa taarifa ya tukio hilo ambalo amelitaja kuwa sio la
kiungwana amesema lilitokea June 9, 2023 majira ya saa mbili usiku .
Kamanda Abwao amesema muuguzi huyo ambaye
aliingia kazini akiwa amelewa pombe alitenda kosa hilo wakati alipopangiwa zamu
ya usiku ya kuhudumu wagonjwa wa nje (OPD) ndipo alipotoka na kwenda chumba cha
wagonjwa wa ndani na kumbaka mama huyo mwenye ujauzito wa karibu kujifungua
ambaye alikuwa anaendelea na matibabu ya ugojwa wa malaria.
Muuguzi huyo alikutwa akiwa na bomba la sindano
pamoja na dawa za usingizi huku taarifa ya kitabibu zikithibitisha kuwa
alimwingilia mgonjwa huyo.
Mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakani mapema hii
leo June 13, 2023 kujibu tuhuma zinazo mkabili baada ya upelelezi kukamilika.
0 Comments