Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kapsumbeiywo huko Kuresoi Kusini, Kaunti ya Nakuru Jumatatu aliuawa baada ya kufumaniwa akilamba asali ya Mke wa mtu mwenye umri wa miaka 35 kwenye kitanda chake cha ndoa.
Mwanafunzi huyo alichomwa kwa panga mara kadhaa na mume wa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina la Japheth Bii.
Akithibitisha kisa hicho, DCIO wa Kuresoi Peter Obonyo alisema mwanafunzi huyo alifariki katika Hospitali ya Nakuru Level Five alipokuwa akipatiwa matibabu.
Polisi wameanzisha msako wa mshambuliaji huyo ambaye alitoroka baada ya kisa hicho.
0 Comments