ASKARI AJARIBU KUJINYONGA BAADA YA KUBAKA NA KULAWITI,ASHIKILIWA NA POLISI


Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala linamshikilia Said Hassan Said(26) Askari Magereza Mkazi wa Ukonga kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka( 29) jina limehifadhiwa

''Mnamo septemba 1,2021 majira ya saa tano na nusu usiku katika barabara ya Madafu Ukonga askari huyo wa Jeshi la Magereza mwenye namba B 9780 WDR Said Hassan akiwa na mwenzake walimkamata kwa nguvu msichana na kumuingiza kwenye gari dogo kisha kuondoka naye hadi kwenye nyumba iliyopo karibu na KMKM Ukonga Magereza na kuanza kumbaka na kumlawiti kwa zamu"

Baada ya kufanya unyama huo watuhumiwa hao waliendelea kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia na kumsababishia majeraha makubwa na maumivu katika sehemu zake za siri.

Mtuhumiwa baada ya kugundua kuwa anatafutwa na Polisi kwa tukio hilo baya alilofanya na mwenzake ,mnamo septemba 2,2021 alifanya jaribio la kujinyonga na kuacha ujumbe wa maandishi kwa mkuu wake wa kazi na askari wenzake kuwa,"Mnisamehe kwa tukio nililofanya nitsonekana nimekufa kizembe " Lakini kabla ya kufanikisha azma yake ya kujitoa uhai alikamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi.

Mtuhumiwa mwenzake ambaye walitekeleza wote unyama huo bado hajakamatwa.

Post a Comment

0 Comments