WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Asajile Mwambambale, ili kwenda kujibu tuhuma zinazomkabili katika Halmashauri ya wilaya ya Kilosa za wizi wa mabati 1,172.
Pia amemuagiza katibu mkuu TAMISEMI kupeleka tume huru ya kuchunguza kwa kina suala hilo
Aidha amewakumbusha watumishi wote wa sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za serikali za mitaa kufanya kazi kwa weledi ,kuwa waadilifu na makini utendaji wao wa kaziwa kila siku.
0 Comments