![]() |
Didier Gomes da Rosa |
Shirikisho la soka Afrika CAF limetoa orodha ya majina ya makocha ambao hawaruhusiwi kukaa kwenye benchi la ufundi katika mechi za mashindano ya klabu bingwa Afrika na kombe la shirikisho Afrika .
Katika orodha hiyo yumo kocha wa klabu ya simba Didier Gomes da Rosa ambaye atatakiwa kukaa jukwaani mechi za CAF Champions League.
CAF wanataka kocha mkuu awe na leseni ya UEFA A PRO ambayo ni sawa na CAF A.
Didier Gomes da Rosa ana leseni ya UEFA DIPLOMA A .
Vyama vya soka vinavyoongoza vilabu tajwa kwenye orodha ambavyo ni TFF ya Tanzania na FERWAFA ya Rwanda vimeshapewa taarifa mapema .
0 Comments