WATU 45 WASHIKILIWA KWA UUZAJI NA USAFIRISHAJI MADAWA YA KULEVYA K'NJARO

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 45 kwa makosa ya uuzali na usafirishaji madawa ya kulevya. 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Simon Maigwa amesema , jeshi hilo limeanzisha operesheni maalum kukamata dawa za kulevya za viwandani na mashambani. 

Kamanda Maigwa ameongeza ,  katika wiki ya kwanza ya operesheni jumla ya watuhumiwa 45 wamekamatwa pamoja na vielelezo ikiwamo pombe haramu ya gongo lita 206, mitambo miwili ya kutengenezea gongo,  mirungi kilo 78 na bangi misokoto 670.

Post a Comment

0 Comments