Kutokana na Ubora wa miundombinu ya uwanja wa Chamazi Complex uliowavutia Horseed FC ,Mchezo wa Mkondo wa Pili wa marudiano Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Horseed FC kutoka nchini Somalia na wawakilishi wa Tanzania, Azam FC utapigwa Jumamosi ya Septemba 18 katika dimba la Azam Complex na si Uwanja wa Uhuru kama ilivyotangazwa awali.
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Azam, Thabit Zakaria "zaka zakazi" amesema Horseed FC wameamua kuomba mchezo huo kurudishwa Chamazi kutokana na ubora wa Uwanja huo katika suala zima la miundombinu.
“Horseed wameamua kuhamishia mechi yetu Azam Complex baada ya mechi yetu ya awali kupangwa kuchezwa Uhuru na sababu kubwa ni wao kuridhishwa na miundombinu iliyopo Chamazi” .
Mechi ya kwanza Azam ilishinda mabao 3-1 wakiwa wenyeji wa mechi hiyo, na mechi ya pili watarudi kama wageni.
Horseed kucheza michezo yao yote Tanzania imetokana na Usalama kutokuwa wa kuridhisha nchini Somalia.
0 Comments