Mtangazaji nguli nchini Salama Jabir jana alitangaza kuachana na kituo cha EATV ambacho amefanya kazi kwa muda wa takribani miaka 19 akidai kuwa anakwenda nje ya media hiyo kuona pia hali ikoje.
Salama amekuwa EATV kwa muda mrefu akijizolea umaarufu zaidi na vipindi kama Mkasi ✂, Shabiki On Saturday (SOS) pamoja na kipindi cha SALAMA NA..
Huko mitandaoni tetesi zimekuwa nyingi kuwa huenda akawa msemaji wa klabu ya Simba SC japo mwenyewe amekanusha kuwa si kweli na kwamba hata yeye anaziona habari hizi kwenye mitandao ya kijamii kama wanavyoona wengine.
Tayari imeshaelezwa kuwa Salama kwa sasa anafanya kazi kwenye Kampuni MultiChoice kupitia king’amuzi chao cha DStv.
0 Comments