Baada ya  Bondia  Mtanzania Tony Rashid kushindwa kuutetea mkanda wa ABU dhidi ya bondia Bongani Mahlangu raia wa Afrika Kusini amefunguka na kusema mpinzani wake anasadikiwa kutumia dawa za kuongeza nguvu.

“Mimi mwenyewe ninashangaa imekuwaje, kwa sababu tangu raundi ya kwanza mpaka ya 12 nilikuwa nampiga, nyote mmeona, lakini kuna kitu kilibadilika ghafla. Uongozi wangu walianza kushtuka tangu mapema kwenye kona yake alikuwa akipewa vitu kama dawa na kutumia, mimi sikujua.

“Zile ni dawa za kuongeza nguvu, haturuhusiwi kutumia dawa za kuongeza nguvu. Lakini tayari tumeshaliwasilisha kwa wahusika na madaktari wamevichukua vile vitu kwa ajili ya vipimo, endapo itabainika alikuwa akitumia dawa basi atanyang’anywa mkanda huo na kuvuliwa ubingwa. Tusubiri majibu tuone.,” amesema Tony.