Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema Upo uwekezekano Simba kucheza na Al Ahly ya Misri iliyochukua taji hilo mara tano, pia wapo TP Mazembe na Raja Casablanca waliochukua mara nne au karata itawangukia Wydad Casablanca ya Morocco iliyotwaa taji hilo mara tatu kama ilivyo kwa Esperance.
“Bado tunaangalia timu itakayotufaa lakini niwahakikishie kwamba tutacheza na timu ambayo imetwaa ubingwa zaidi ya mara tatu tena ule wa Afrika.“Kuelekea kwenye Simba Day tutatumia slogan ya ‘One Team, One Dream tukimaliza na Asubuhi Tu, Twendeni Wenye Nchi’. Pia kutakuwa na Wiki ya Simba ambayo itaanza Septemba 13 mpaka siku ya kilele Septemba 19.”
0 Comments