Katika maisha ya mahusiano ili uishi kwa amani jifunze kuishi kama mjinga ,Bora uonekane mjinga ili moyo wako uendelee kuwa na amani Hata kama unahisi ana kusaliti muache usihangaike kutafuta ushahidi.

Usijifanye wewe ndo unajua sana kupenda kiasi cha kutaka kuangalia kila sms na simu inayo ingia kwake Utakayokutana nayo utaishia kujuta 

Epuka maisha ya kumfuatilia mtu unaempenda maana utaishia kuumia. Hata ukague simu yake au akaunti yake ila kuna namna anavyo wasiliana nao. 

Msaliti siku zote ana roho ya ujasiri maana haoni shida kukuzunguka hapo hapo. Kuna wakati unayemsimulia ndiye mwizi wako.Huenda rafiki au ndugu yako ndiye anaiba au Huenda mtu chumba jirani ndiye .mwizi wako.

Huwezi kumzuia msaliti maana ana mbinu nyingi kujihami. Kama sio wako hawezi kuwa wako hata uchunguze sana mtaishia kugombana na kisha kuachana,Kama ni fungu lako hata uwe mbali bado atajitunza kwa ajili yako.

Kupeana password za mtandaoni haimanishi kuwa ndio upendo wa dhati. Wala sio kigezo cha uaminifu na epuka kujisifia kuwa mtu wako ametulia maana wanao faham nyendo zake wana kuchora tu.

Jiamini kwanza wewe ndipo muamini mwenzako