Klabu ya Mtibwa Sugar kutoka kule Manungu Morogoro, katika taarifa yake iliyotolewa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Mtibwa imesema;
"Tumefanikiwa kuinasa saini ya beki wa kati mwenye ufundi mkubwa Sana na hadhi ya nchi Abdi Banda. Tumemsajili Banda kutoka katika klabu Ts Galaxy inayoshiriki ligi kuu Afrika Kusini".
Banda alipoulizwa amesema, “Ujue mimi nilikuwa Sauzi kama mwezi hivi, nilifanya nao mazoezi wiki tatu na baada ya hapo wakaniambia mwenye timu hayupo nimsubiri mpaka aje,” alisema Banda na kuongeza;
“Wakati nikiwa namsubiri huku ikienda wiki ya nne nikapata Uviko 19 nikawekwa tu ndani mpaka nikae sawa, nilipokuja kukaa sawa wakaniambia wanipe tena wiki mbili zingine kitu ambacho niliona kama hawana nia na mimi.”
Mpaka sasa Mtibwa imewanasa Said Ndemla kwa mkopo kutoka Simba, kiungo George Chota na beki Abdi banda.
0 Comments