Na Rehema Abraham
Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za wanawake nchini Tanzania yameungana kwa pamoja kuadhimisha wiki ya mwanamke aishie Kijijini kwa kutembelea baadhi ya mikoa kuelimisha haki ya mwanamke ya kumiliki ardhi kwani imeonekana kuwa wanaume wamepewa kipaumbele kutokana na mifumo dume iliyopo katika jamii.
Aidha katika kuadhimisha siku hiyo wadau hao wamelazimika kupita kwenye baadhi ya Mikoa hapa Nchini kwa ajili ya kutoa Elimu na kuhamasisha wanawake kufahamu haki zao katika umiliki wa ardhi na kuona ni changamoto zipi wanazokumbana nazo katika kipindi hiki Cha ugonjwa wa UVIKO 19.
Mashirika hayo ni pamoja na chama cha wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA), (LANDESA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia ,wazee na watoto .
Akizungumza katika viwanja vya pasua mkoani Kilimanjaro Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogolo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai amesema kuwa suala la umiliki wa ardhi kwa wanawake mkoani humo Bado upo chini kutokana na mfumo dume wa wanaume kumiliki ardhi tofauti na mwanamke .
Mpogolo amesema miongoni mwa mikoa yenye changamoto juu ya kina mama kumiliki ardhi Mkoa wa Kilimanjaro ni moja wapo na kusema inasababishwa na uchache wa ardhi hali ambayo hupelekea wanaume kumiliki kuliko wanawake.
Katika utoaji wa elimu wameanza mkoa wa Mwanza-Misungwi, Babati na Arusha ambapo katika mikoa hiyo wameweza kuwaeleza umuhimu wa mwanamke wa kijijini anavyokuwa na thamani kubwa kwenye jamii hususani umilikishwaji wa ardhi .
Bi.Fatma Kimwaga wakili na mratibu kutoka Chama cha wanasheria wanawake Tanzania TAWLA amesema kuwa katika kuadhimisha siku ya mwanamke wa Kijijini wamekuwa wakipokea malalamiko ya changamoto ya wanawake kutomiliki ardhi kwa sababu hawana fedha pamoja na mfumo dume ambao umekuwepo hapo nyuma.
"Katika jamii nyingi inaonekana mwanaume ndio anayepaswa kumiliki ardhi lakini pia kutokana na mfumo dume wanawake hao wameshindwa kumiliki ardhi kihalali, ukiangalia pia changamoto nyingine ambayo wanawake wanakutana nayo utakuta mwanaume anakufa lakini ndugu wa Mume wanakuwa wanamnyanyasa ,wanamtoa kwenye nyumba hivyo anakosa haki yake ya msingi" Kimwaga,
Hata hivyo Katika utoaji wa elimu wameanza mkoa wa Mwanza,Misungwi, Babati na Arusha ambapo katika mikoa hiyo wameweza kuwawaleza umuhimu wa mwanamke wa kijjijni anavyokuwa na thamani kubwa kwenye jamii hususani umilikishwaji wa ardhi na
Kauli mbiu katika kuadhimisha siku ya mwanamke wa Kijijini ni" ARDHI NI NYENZO YA MAENDELEO KWA MWANAMKE WA KIJIJINI.
0 Comments