MBUNGE AFURAHISHWA NA MWITIKIO WA CHANJO UVIKO-19



MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Vijijini Michael Mwakamo amewashukuru wananchi wa Jimbo hilo kwa kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 baada ya dozi 2,000 zilizotolewa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kuisha.

Pongezi hizo amezitoa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mlandizi juu  ya masuala mbalimbali ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa ambapo amesema uhamasishaji ndiyo umefanikisha kuiisha kwa dozi hizo.

Mwakamo amesema tayari wameshapeleka maombi kuongezewa dozi nyingine ili kwa wale waliobakia nao wapate chanjo hiyo.

Post a Comment

0 Comments