Kaimu Mkurugenzi Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI Kihinga iliyoko mkoani Kigoma Dkt. Filson Kagimbo amesema Tanzania kuna aina tatu za chikichi ambazo zipo za kienyeji dula(jiwe) zinapatikana kwa asilimia 90, pisifera(bubu) zinapatikana kwa uchache chini ya asilimia 0.01 na hii ya kisasa ambayo inaitwa tenera(hote) ambayo inapatikana kwa asilimia 9.9 hizi ni aina tatu ambazo zinapatikana duniani kote.
Amesema uzaaji wa zao la chikichi aina ya dula hutoa mafuta kidogo wastani wa 1.6 kwa hekta huku aina ya pisifera haipatikani kwa urahisi na haikamuliwi mafuta lakini pia ni chache sana unaweza kuwa na shamba la hekali moja lakini ukakosa mti hata mmoja wa bubu.
Aina ya mbegu ya Tenera inapatikana kwa asilimia 9.9 ambapo ukilima unapata tani 4-5 kwa hekta ndio maana serikali inahamasisha wakulima kutumia mbegu hiyo ambayo imeonyesha kuwa msaada mkubwa katika utatuzi wa uhaba wa mafuta nchini.
“Kwanini tunasema kuwa ni mbegu bora tunaangalia vitu viwili ukipanda Tenera inaanza kuzaa baada ya muda mfupi yaani baada ya miaka miwili hadi mitatu unaanza kuvuna tofauti na dula ambayo ukipanda unaanza kuvuna baada ya miaka 5-7 ndio maana tunaiita bora” Dk Kagimbo
“Ukitaka kulima kwa tija inakubidi ulime tenera ambayo ndio inaweza kuongeza na kukuza uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla kwa sasa tunalima eneo la mchikichi hekta 30,000 ambayo tunapata tani 40,000 za mafuta uwezo wetu kwa mazao yote ni tani 240,000 ambapo ukiangalia mchikichi mchango wake unaonekana ni mdogo ndio maana tunalenga kuongeza mafuta kwa kutumia mchikichi kwakuwa ni zao ambalo linaaminika duniani kwa kutoa mafuta mengi”
“Mfano ukilima alizeti hekta moja unapata tani 0.8 ukilinganisha na mchikichi utaona jinsi gani inazidi alizeti kwa upatikanaji wa mafuta ndio maana serikali imeona iwekeze kwenye zao hili ambapo asilimia zaidi ya 80 inatokana”
“Tanzania kwa mwaka 640,000 mafuta ya kula sisi asilimia 37 tu ndio tunazalisha ili upate zote kwenye mchikichi inabidi ulime hekta 150,000 ambapo utahitaji miche milioni 20,000 ili upande eneo lote,sisi tumeanza kuzalisha ambapo tumezalisha miche milioni 7265 tutahitaji miaka 3”
“Tukifanikiwa tutakuwa tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini kumbuka yapo mazao mengine yanayotoa mafuta pia ambayo ni pamba, ufuta, karanga na alizeti”
“Kwa magonjwa yote yanafanana kwasababu aina hii mpya tumechavusha kutoka kwenye aina dula na pisifera ndio maana zinafanana kwa tabia na kushambuliwa na wadudu na magonjwa”
“Bei ya chikichi imetofautiana kulingana na msimu ambapo kuanzia mwezi wa tisa hadi wa tatu mavuno yanakuwa mengi na bei zinakuwa nafuu huuza lita kwa 1500 lakini wakati ambao sio wa msimu huuzwa 2000 lakini baada ya serikali kuhamasisha uhamasishaji wa michikichi bei imepanda hadi kufikia shilingi 3000”
“Unajua haya mafuta ya safi, korie, mukwano yote ni mafuta ya mawese lakini wengi hawajui na yana bei kubwa sana kuliko mafuta yenyewe ya asilia” amesema Dk Kagimbo
Nae Mkurugenzi wa uhaurishaji teknolojia na mahusiano kutoka Tari Juliana Mwakasendo amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa tunatoa teknolojia zote zilizo na watafiti wetu na kuzifikisha kwa watumiaji.
Sisi tunahakikisha kuwa teknolojia zote tunazitoa kwenye makabati na kuzipeleka kwa watumiaji kwanini tunazipeleka tumeona tija ni ndogo kwenye mazao mbalimbali tunapopeleka tija tunaona maboresho katika kilimo
Viwanda vingi asilimia 65 wanatumia mazao sisi kama tari lazima tutumie fursa zilizopo nchini ili kuhakikisha kuwa wadau mbalimbali wamepata elimu stahiki ili kuweza kunufaika kwenye mnyororo wa thamani
“Sio tu wadau tuna vituo nane ambavyo vinatumika kwaajili ya kutolea elimu kwa wakulima mbalimbali kwa mwaka mzima hata hivyo kupitia vyombo vya habari vipeperushi mbalimbali tunaweza kutoa elimu mbalimbali” alisema Mwakasendo
Nae Tatu Ramadhani mkulima wa zao la chikichi wilayani kigoma amesema kuwa serikali imeonyesha nia ya kuwasaidia katika kuinua zao la chikichi hivyo wanaamini kuwa wataweza kufanya mambo makubwa zaidi kwenye zao hilo.
0 Comments