MAHUSIANO yana jengwa na mawasiliano pia kujiamini na kumuamini unae mpenda.

Unaweza mpenda  mtu ambae hujawahi/hamjawahi kuonana ila mawasiliano yenu yanaweza kuwa mazuri kuliko yule unaemuoona kila Siku.

Maamuzi yako ndiyo furaha yako ,Uvumilivu wako utakupa chaguo lako ,Penda CHAKO punguza tamaa zako

Kuwasiliana iwe kwa simu au text  ilimradi Mara kwa Mara basi  hufanya muthaminiane na kukumbukana ,usiogope kumpenda kisa yupo mbali nawe au kisa bado hujamuona ili mradi kila MTU anapicha ya mwenzake na kazi ya mwenzake basi mwaweza endelea na mipango yenu mpaka mda wa kukutana utapokafika.

Usaliti ni tabia ya MTU hata unaeishi nae chumba kimoja bado anaweza ingia chumba cha jirani wakati wewe umelala.

Tambua kuwa rafiki yako au jirani yako wa mtaa au wilaya moja anaweza kukusaliti kwa mpenzi wako

Sio kila aliyembali BASI ukajua anafanya usaliti maana wengine wanajiheshimu na ngono kwao sio muhimu sana ndo maana wanaweza kukaa MDA mrefu bila sex.

Yupo MBALi nawe na Hujawahi au umewahi kumuona Jitunze kwa ajili yake,Endelea kumpenda na kumuamini mpaka utapokutana nae.

Ila kama unapenda sana ngono basi usianzishe mahusiano na mtu wa mbali