Ugumu wa maisha usikufanye utamani KUOLEWA haraka ukiamini utapata nafuu kwamba unaweza kula na kulala bure kwa mumeo badala yake unaweza ukawa unaishi kwa mashaka na simanzi mda wote.
Atakuvisha na kukulisha ila anaweza kukudharau kwa kuwa alikukuta upo tu kwenu hata mtaji wa genge la 50 elfu huna.
Jishughulishe jifunze kujitegemea ndo njia rahisi kuishi kwa furaha katika MAHUSIANO mwanamke ukiwa na kaz yako.
Pia kumbuka sio kila mwanaume anapenda mwanamke MWENYE kazi wengine wanataka tu uwe mama WA nyumbani sasa ukikubali kufanywa yaya tegemea majuto mbele.
NDOA ni jambo la heri lililopangwa na Mungu, kwahiyo ambao bado tusiogope kwa kuwa wengi wanalia na ndoa zao maana wao na wewe mpo tofauti kwani nawe una fungu lako.
Kuachwa au kusalitiwa na uliye mtegemea sio mwisho wa safari yako ya kupata NDOA chamsingi endelea kumwomba Mungu siku utapata aliye bora kuliko hata aliyekuacha.
Huyu anapoachwa au kuachika , mwingine anaoa au kuolewa.
Kila mtu ana fungu lake usiogope simulizi za wengi walioteseka na ndoa zao,jaribu bahati yako,Tusikate tamaa na wala tusiendekeze anasa wakati tuna mengi ya kufanya.
Uliye nae bado huna uhakika kama ndiye Mkeo au mumeo wa kesho maana nae Mungu ana mipango yake Mnaweza kutenganishwa na kifo au usaliti hata hisia za upendo kuisha..
Kuna watu wamepata wake wazuri kwa sura na umbo ila hawawezi kusimama kama Mke au Mama ,Pia kuna wanawake wamepata kuolewa na wanaume watanashati na wenye mafanikio ila dharau na usaliti ndo mahala pake.
Kumbe usiweke kigezo cha uzuri wake au mali na elimu ila angalia kama atakufaa kujenga familia.
0 Comments