Katibu tawala Wilaya ya Ulanga Abraham Mwaikwila

Wananchi wa kitongoji cha Mikoroshini kata ya Minepa eneo la Iluma Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro wameiomba serikali kukidhibiti kikundi cha watu wanaojiita mgambo maarufu kama VILAPU ambao wanafanya uvamizi katika makazi ya wananchi hao na kufanya uharibifu ikiwa ni pamoja na kuwapiga,kupora kisha kuchoma nyumba zao. 

Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao wamesema VILAPU wamekuwa wakiwavamia usiku kisha kuanza kuwapiga huku wakijifanya ni askari wa Wanyamapori.

Wananchi hao wamesema kufuatia kadhia hiyo wametoa taarifa kwa baadhi ya viongozi akiwemo diwani lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ya kudhibiti kikundi hicho kinachojulikana kwa jina la VILAPU.

Mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham  amethibitisha kuwepo kwa matukio ya wananchi wanaoishi maeneo Iluma kuharibiwa mali zao  pamoja na kupigwa na VILAPU.

Kwa upande wake Katibu tawala Wilaya ya Ulanga Abraham Mwaikwila amewataka watu wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwa wananchi hao kuacha mara moja huku akiahidi kulifanyia upelelezi wa kina jambo hilo.

TAARIFA KAMILI HII HAPA ,BOFYA