Benki Kuu imesema itaanza kuwachukulia hatua wote watakaohusika na vitendo vya matumizi mabaya ya noti ikiwemo kuweka pesa sakafuni na sehemu yoyote ambayo sio nadhifu kwasababu vitendo hivyo vinasababisha uchakavu wa fedha na kuiongezea Serikali gharama kubwa za kuchapisha fedha.
Hatua hii inakuja kufuatia hivi karibuni kuibuka kwa wimbi la Watu kutunza Wahusika wa matukio hususani kwenye sherehe za harusi kwa kuwarushia noti na zinaanguka sakafuni na muda mwingine kukanyagwa.
0 Comments