MBUNGE WA MADABA DKT.MHAGAMA APIGANIA BARABARA IPANDISHWE HADHI.


Mbunge wa Jimbo la Madaba Dkt Joseph Mhagama akiiomba Tanroads mkoa wa Ruvuma kuipandisha hadhi barabara ya Wino,Ifinga hadi Imalinyi ya mkoa wa Morogoro.

NA AMON MTEGA,SONGEA .

MBUNGE wa Jimbo la Madaba Dkt,Joseph Mhagama amewaomba Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)mkoani Ruvuma kuichukua na kuipandisha hadhi barabara inayoanzia kata ya Wino,Ifinga hadi Imalinyi ya mkoa wa Morogoro ili iweze kufanyiwa kazi kwa haraka zaidi.

Ombi hilo amelitoa wakati akichangia hoja mbalimbali kwenye kikao cha bodi ya barabara Mkoani humo ambacho kimehudhuliwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wabunge wa Majimbo ya mkoa huo .


Dkt Mhagama amesema kuwa awali barabara hiyo imekuwa ikihudumiwa na Wakala wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA)jambo ambalo ilikuwa inashindwa kufikiwa malengo kutokana na ufinyu wa bajeti kwenye kitengo hicho.

Mbunge Dkt Mhagama akichangia hoja na kujenga hoja juu ya barabara hiyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Balozi Wilbert Ibuge amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa inaunganisha mkoa wa Ruvuma na Morogoro .

Ameongeza kuwa licha kuunganisha mkoa wa Ruvuma na mkoa wa Morogoro bado itasaidia watalii kufika kirahisi kutokana na maeneo mengi ya barabara hiyo ina vivutio ambavyo vitaliongezea pato taifa pamoja na mkoa kwa ujumla .

Mbunge wa Jimbo la Songea mjini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro akiiambia Tanroads ya mkoa wa Ruvuma kutilia mkazo barabara zinazopita kwenye vivutio vya utalii kama barabara ya Wino,Ifinga hadi Imalinyi ya mkoa wa Morogoro.

Naye mbunge wa Jimbo la Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt,Damas Ndumbaro akichangia hoja ya barabara hiyo amesema kuwa ni moja kati ya barabara ambazo zinatakiwa kuwekewa vipaumbele kwa kuwa itakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa kutoka na vivutio vilivyopo na vivutio vingi vya utalii vinashindwa kufikiwa kutokana na kukosa barabara.


Kwa upande wake meneja wa Tanroads mkoa wa Ruvuma mhandisi Ephatar Mlavi akipokea ombi hilo amesema ataenda kulifanyia kazi kwa kufuata taratibu za miongozo ya namna ya kuzipandisha hadhi barabara kama hiyo ya Wino,Ifinga hadi Imalinyi iliyopo mkoa wa Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Wilbert Ibuge akizungumzia umuhimu wa kuongeza barabara katika mkoa huo na kuufanya ufunguke kwa kasi.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Wilbert Ibuge ambaye amekuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa malengo ya mkoa huo ni kuwa na barabara nyingi ili kuufanya mkoa uweze kufunguka kwa kasi zaidi.

Post a Comment

0 Comments