TATUA MAISHA YAKO KWA MASWALI HAYA


KWA NINI?

Kwa nini udharaulike?
Kwa nini usahaulike
Kwa nini uonewe?
Kwa nini usalitiwe
Kwa nini usipendwe?
Kwa nini ukandamizwe?

AU

KWA SABABU
Wewe maskini
Huna kazi
Huna elimu
Huna mvuto
Huna ushawishi
Huna mchango kwake/kwao

Vyovyote itakavyo kuwa
Usiruhusu mtu au watu wakudharau sababu ya hali yako kiuchumi au kijamii Siku zote jiamini Na jithamini kisha jikubali vile ulivyo

Usijione mnyonge kudharauliwa katika familia kisa huna pesa huku wadogo zako wakinyenyekewa sababu ya pesa zao.

Tengeneza mazingira watu wakuelewe na kukuheshimu vile ulivyo.. Sio lazima ushindane nao,pita njia yako... Mtu ambae atakuamini na kukuvumilia ulivyo leo ndiye RAFIKI au MPENZI wa thamani

Juhudi na kujiamini kwako ndiko kutakufanya siku nawe uheshimiwe.

Kama wao wanajiona warembo au handsome kukuzidi,mbona hawana ndoa? Mbona ndoa zao hazina amani?

Wana pesa zaidi yako lakini hawana furaha na Amani uliyo nayo.

Wamesoma kukuzidi lakini hawana kazi,hawana kipato kama Chako

Hivyo maisha ya watu yasikuumize kichwa ,tengeneza yako wengine wayatamani.

Post a Comment

0 Comments