Breaking News: Ajali yaua 19,Kujeruhi Mafinga-Iringa


Jumla ya watu 19 wamefariki dunia na wengine 8 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Lori aina ya Scania na Coster iliyotoka eneo la Changalawe wilaya ya Mufindi mkoani Iringa alfajiri ya leo.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Scania yenye namba za Usajili T 736 AAE na Coaster yenye namba za usajili T542 DQV


Akitoa taarifa kwa mkurugenzi wa mji wa Mafinga, mganga mfawidhi wa hospitali ya Mafinga Dr. Victor Msafiri amesema ajali hiyo iliyotokea imesababisha vifo vya watu 19 na majeruhi ambao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo.


Amesema Majeruhi wanaendelea kupata matibabu na baadhi ya miili ya marehemu imeshatambulika na mingine inaendelea kutambuliwa na jeshi la polisi


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafinga mji Bi, Happiness Laizer amewatembelea majeruhi na kuwapa pole huku akiwaomba madaktari kuwapa huduma stahiki ili hali zao ziweze kutengemaa.

Post a Comment

1 Comments