PROFESA JAY ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI.



Msanii nguli wa muziki wa bongo fleva Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya Hali yake kiafya kuonekana kuimarika.

Profesa Jay ambaye alilazwa hospitali ya taifa Muhimbili ameruhusiwa Jana baada ya kukaa hospitali Kwa takribani siku 127 za matibabu katika hospitali hiyo.

Taarifa ya kuruhusiwa Kwake imetolewa na hospitali ya taifa ya Muhimbili yenyewe katika ukurasa wakewa  mitandao ya kijamii wa Instagram.

Post a Comment

0 Comments