KOCHA MPYA SIMBA HUYU HAPA


Baada ya Shirikisho la soka Afrika  CAF kutoa orodha ya majina ya makocha ambao hawaruhusiwi kukaa kwenye benchi la ufundi katika mechi za mashindano ya klabu bingwa Afrika na kombe la shirikisho Afrika ambayo imemgusa kocha wa klabu ya simba Didier Gomes da Rosa  mwenye  leseni ya UEFA DIPLOMA A ,KLABU ya Simba imemteua Thierry Hitimana (42) kuwa kocha msaidizi ikiwa ni hatua ya kuimarisha benchi lake la ufundi ili kuhakikisha inafanya vizuri zaidi kwenye michuano mbalimbali ambayo itashiriki.

CAF wanataka kocha mkuu awe na leseni ya UEFA A PRO ambayo ni sawa na CAF A.

Thierry ni mmoja wa walimu wanaoheshimika Rwanda na aliwahi kuwa msaidizi wa Didier Gomez wakati Rayon Sports ikitwaa ubingwa wa ligi kuu nchini humo.

Mrwanda huyo ni msomi wa shahada ya Uzamili katika masuala ya Fedha aliopata nchini Ubelgiji pia ana leseni ya ukocha daraja A inayotolewa na CAF.

Simba ambayo inatetea ubingwa wa ligi msimu huu imejipanga pia kufanya vizuri kimataifa baada ya msimu uliopita kutupwa nje na Kaizer Chiefs ya Afrika kusini kwa mabao 4-3 katika hatua ya robo fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments