Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa Morogoro limetoa msaada wa vyakula mbalimbali katika kituo Cha kulelea watoto yatima Cha Dar_UL_Muslim Morogoro .
Akizungumza Mara baada ya kukabidhi msaada huo kamanda wa jeshi hilo mkoa Morogoro Goodluck Zelote amesema wameona Ni vyema kuwakumbuka watu wenye uhitaji hasa kipindi Hiki Cha sikukuku ili nao washeherekee Kama watu wengine
Kamanda Zelote amesema jeshi hilo lina nafasi pia ya Kushirikiana na jamii ili kupata urahisi wa utendaji kazi wake
Kamanda Zelote ameongeza kwa kusema kuwa watoto wanapaswa kupata elimu ya uokozi tangu wakiwa wadogo hivyo wazazi na walezi wanajukumu la kutoa elimu hiyo kwa kuwatajia namba ya dharura 114 ili waikariri.
Katika hatua nyingine kamanda Zelote amewataka wazazi kuwa makini katika kipindi hiki Cha sikukuu ili kuepuka ajali zisizo za lazima pia akitoa Rai kwa watu wanaohitaji kupiga milipuko wafike katika kituo Cha jeshi Hilo ili kupata kibali maalum
Kwa upande wake Mlezi wa kituo hicho Ashura Rashird amelishukuru jeshi hilo Kwa msaada huo na kuomba taasisi zingine kuiga mfano huo.
Kituo hicho kimeanzishwa mwaka 1994 kina zaidi ya watoto 70 na kina hudumia watoto wa jinsia zote .
0 Comments